- 10,211 viewsDuration: 2:21Makachero wa DCI wamewakamata washukiwa wawili kuhusiana na uchunguzi wa mauaji ya Daktari wa maradhi ya akili, Victoria Nthunya Mutiso, aliyekuwa mkurugenzi katika shirika la utafiti wa afya ya akili na ubongo. Waliozuiliwa ni Rose Mbithe Mulwa, aliyekuwa mke wa Profesa David Ndetei, pamoja na mwanawe, Chris Mulwa. Polisi wanasema walipata vielelezo muhimu wakati wa operesheni ya kuwakamata, ambavyo vinaendelea kufanyiwa uchunguzi. Aidha, polisi wanaamini kuwa mgogoro wa kipande cha ardhi chenye thamani ya mabilioni ya pesa huenda ndio chanzo cha mauaji hayo. Franklin Wallah ana taarifa zaidi.