- 7,125 viewsDuration: 2:53Baadhi ya wazazi katika Shule ya Wasichana ya St Georges hapa Nairobi sasa wanataka uwajibikaji na haki kwa watoto wao wakidai kuwa haki zao zilikiukwa wakati wa msako uliofanyika shuleni. Wazazi hao wanadai kuwa baadhi ya wanafunzi waliguswa isivyofaa katika sehemu zao za siri wakati wa zoezi hilo. Usimamizi wa shule hiyo umeomba radhi kwa wazazi kufuatia madai hayo ya ukiukaji.