- 2,005 viewsDuration: 1:09Mwanasiasa Ali Adan Abdi amepokea rasmi uungwaji mkono kutoka kwa wazee wa ukoo wa Adola pamoja na wanajamii wa Garre katika mkutano uliofanyika Banisa, Kaunti ya Mandera. Uidhinishaji huo unaonekana kuwa hatua muhimu katika azma yake ya kuwania kiti cha ubunge wa Banisa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Mkutano huo pia uliangazia utaratibu wa jadi wa mashauriano unaotumiwa na jamii hiyo, ambapo maamuzi kuhusu uongozi hufanywa kupitia majadiliano ya kifamilia ndani ya ukoo Wadau wa kisiasa wanaamini kuwa mazungumzo hayo ya ndani yatakuwa na mchango mkubwa katika kuamua ni nani atakayepata baraka za jamii kupeperusha bendera ya kuwania kiti hicho na mashauriano ndani ya jamii kuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua mwelekeo wa siasa za eneo hilo kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027.