- 8 viewsWazee kutoka ukoo mkubwa wa Karayu wa jamii ya Borana katika Kaunti ya Isiolo wamepinga vikali kuanzishwa kwa kamati ya kuiongoza jamii hiyo inayodaiwa kubuniwa na rais, wakisema hatua hiyo inakinzana na mila na desturi za jamii hiyo ambazo zinatambua mfumo wa asili wa kidemokrasia wa uongozi unaojulikana kama Mfumo wa Gadha.