- 150 viewsDuration: 1:52Wazee wa jamii za wafugaji kutoka kaunti za laikipia , isiolo na samburu ambazo zimekuwa na utamaduni wa kuibiana mifugo, sasa wameanza kuhamasishana kuhusu jinsi ya kuasi mila hii ili kumaliza wizi wa mifugo katika maeneo yao. Wazee hao Wamekubaliana kutowapa vijana warani idhini ya kuingia katika rika la wazee wa makamu ama kuoa hadi wakome kuiba mifugo. aidha, wanazipongeza idara za usalama kwa kufanya operesheni ya kuwafurusha wezi wa mifugo kutoka msitu wa mukogodo.