- 592 viewsDuration: 2:21Waziri wa afya Aden Duale ametia saini mkataba wa shilingi bilioni 10 na shirika la Beginnings Fund ili kupiga jeki afya ya mama na mtoto. Mkataba huo uatakaodumu miaka mitano utaimarisha huduma za afya kwa kina mama wajawazito ili kupunguza vifo vya wanawake wakati na baada ya kujifungua. Shirika hilo la Beginnings fund litagharamia utekelezwaji wa mradi huu ambao unalenga hospitali 200 katika kaunti 21. Aidha, Duale amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza mageuzi ya sekta ya afya kwa kuimarisha huduma za afya ya msingi.