- 972 viewsDuration: 1:13Kampuni ya kiunzi cha teksi mtandaoni ya Weego imeadhimisha mwaka mmoja wa biashara zake nchini, huku hafla hiyo ikiwapa wateja nafasi ya kupata bei nafuu za safari. Kupitia hafla ya Park & Vybe, kampuni hiyo iliwaandalia abiria wake jioni ya muziki, chakula na dansi, mbali na mafunzo ya kuendesha gari kwa usalama. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa Weego Anthony Macharia amesema kampuni hiyo inaendelea kujivunia kukua na kuwa mojawapo ya teksi bora za mtandaoni nchini.