Skip to main content
Skip to main content

Wetangula asema baadhi ya wastaafu wanapanga kugawanya Magharibi

  • | Citizen TV
    1,951 views
    Duration: 1:48
    Viongozi wa Kenya Kwanza wakiongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula wamesema kuna baadhi ya wanasiasa waliostaafu wanaolenga kuugawanya mkoa wa Magharibi kama njia ya kupunguza ushawishi wa Rais William Ruto, wakisisitiza kuwa mpango huo hautafanikiwa. Akizungumza katika hafla iliyowaleta pamoja viongozi wa eneo la Magharibi huko Chekalini, kaunti ya Kakamega, Wetangula alisema kuna haja ya kudumisha umoja wa kisiasa katika eneo hilo. Wakati huohuo, ameitaka Wizara ya Elimu kuhakikisha inabuni mikakati kabambe ya kuimarisha usalama wa wanafunzi katika shule zote nchini, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kuzuia matukio ya kiusalama shuleni.