Skip to main content
Skip to main content

Wizara ya Afya yahakikishia Wakenya kuhusu utayari dhidi ya Ebola

  • | Citizen TV
    559 views
    Duration: 2:24
    Wizara ya Afya nchini imesisitiza kuwa Kenya imejipanga kikamilifu kukabiliana na ugonjwa wa Ebola iwapo utaripotiwa nchini. Katika taarifa yake, Waziri wa Afya Aden Duale amesema hali nchini Democratic Republic of the Congo inatia wasiwasi kutokana na mwingiliano wa wasafiri katika ukanda huo. Kama anavyoarifu mwanahabari Emily Chebet, World Health Organization imesema mlipuko wa sasa wa Ebola nchini DRC huenda ulikuwa ukienea kwa miezi kadhaa bila kugunduliwa kabla ya kutambuliwa rasmi.