Skip to main content
Skip to main content

Zaidi ya shule 10 ya msingi katika eneo la Nyatike zazindua progamu maalum ya kupanda miti

  • | Citizen TV
    147 views
    Duration: 1:42
    Shule zaidi ya 10 za msingi katika Kaunti Ndogo ya Nyatike zimezindua programu ya kupanda miti inayolenga kukuza hulka ya uhifadhi wa mazingira na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika eneo hilo. Mpango huo, unatekelezwa chini ya programu ya “Adopt a Tree” ambapo kila mwanafunzi anatarajiwa kupanda na kutunza mti hadi ukomae. Walimu waliohusika katika awamu ya majaribio wanasema programu hiyo itasaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira wakiwa wadogo..