- 4,534 viewsDuration: 2:39Zaidi ya watu 200 waliokamatwa jijini Nairobi jana kwa kushiriki maandamano ya kupinga bei ya juu ya mafuta walifikishwa mahakamani leo, huku baadhi yao wakiachiliwa kwa dhamana. Mamia wengine pia walifikishwa katika mahakama mbalimbali nchini kuhusiana na kushiriki mgomo huo. Katibu wa Usalama Raymond Omollo amesema Kamanda wa Kituo cha Polisi cha Nairobi Central, Dishon Angoya, anachunguzwa kufuatia madai ya kuwaachilia mahabusu waliokamatwa wakati wa maandamano.