Familia ya mshukiwa aliyekamatwa Kisii kwa kupotea kwa watoto Langas ajitenga na tuhuma hizo

  • | K24 Video
    49 views

    Familia ya mshukiwa aliyekamatwa Kisii kwa madai ya kuhusika na kupotea kwa watoto Langas , Eldoret imejitokeza na kujitenga na tuhuma hizo. Petronilla Kwamboka alikamatwa baada ya kuhusishwa na kupotea kwa mtoto huko Langas lakini familia yake imejitokeza na stakabadhi kuthibitisha kwamba mtoto aliyepatikana sio mmoja kati ya watoto waliopotea eneo hilo. Haya yanajiri huku hakimu mkuu wa mahakama ya Eldoret dennis mikoyan akimuachilia mshukiwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tano. Polisi nao walimpeleka mtoto kwa uchunguzi wa dna ili kubaini wazazi wake halisi.