Mzozo wa afya Kericho : Madaktari kuanza mgomo mwezi ujao

  • | KBC Video
    5 views

    Chama cha madaktari, wataalam wa dawa na madaktari wa meno kimetoa ilani ya siku 14 ya mgomo kwa serikali ya kaunti ya Kericho, kikilalamikia kutotekelezwa kwa mikataba ya makubaliano kuhusu utendakazi na maagano ya kurejea kazini iliyotiwa saini tarehe 4 mwezi Mei mwaka 2023.Akizungumza katika hospitali ya matibabu maalum ya Kericho, katibu wa tawi la Kericho la chama hicho Stephen Omondi, alionya kuwa huduma za matibabu zitalemazwa kuanzia tarehe 3 Mwezi Machi iwapo serikali ya kaunti itashindwa kutekeleza matakwa yao . Omondi alitaja ukosefu wa bima ya matibabu na kutopandishwa vyeo kwa wahudumu wa matibabu kama baadhi ya malalamishoi wanayotaka yashughulikiwe. Aliwahimiza viongozi wa serikali ya kaunti kuchukua hatua ya haraka kuzuia mzozo katika sekta ya afya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive