Atwoli ashinikiza mitandao ya kijamii idhibitiwe

  • | Citizen TV
    479 views

    Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amekashifu kutotekelezwa kwa nyongeza ya mishahara ya asilimia sita ambayo iliidhinishwa mwaka jana. Atwoli amewakashifu waajiri kw akukiuka agizo la rais kuhusu nyongeza hiyo akisema kuwa hatua hiyo inawadhulumu wafanyikazi. Kwenye maadhimisho ya leba dei hii leo, atwoli pia ameshinikiza kudhibitiwa kwa mitandao ya jamii akisema kuwa hatua hiyo itahakikisha kuwa taifa limestawi na halikabiliwi na misukosuko.