Walimu wakuu walilia pesa za wanafunzi

  • | Citizen TV
    148 views

    Shule za sekondari za umma zinakabiliwa na hali ngumu huku shughuli nyingi zikitatizika kutokana na ukosefu wa umma. Hali hii imesababishwa na kucheleweshwa kwa fedha za ufadhili zinazotolewa na serikali. Mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu wa shule za sekondari - KESSHA- Willy Kuria, amesema kuwa wizara ya elimu ilitoa shilingi 8,319 kwa kila mwanafunzi katika awamu ya kwanza ya ufadhili wa muhula wa kwanza badala ya shilingi 11,122. walimu wakuu hawajapokea ufadhili uliosalia wa muhula wa kwanza na ufadhili wa muhula wa pili. Kuria anasema kuwa hali hiyo inatatiza shule za umma kwani muhula wa pili una shughuli nyingi zaidi.