Shughuli za biashara zimetatizika mjini Kilgoris

  • | Citizen TV
    459 views

    Shughuli za biashara zimetatizika katika mji wa Kilgoris baada ya gari la maafisa wa GSU kudaiwa kumgonga na kumuua mhudumu wa boda boda. Vijana wenye hasira waliwasha moto na kufunga barabara. Inadaiwa kuwa gari lililomgonga mhudumu huyo wa bodaboda lilitoroka. mhudumu huyo aliuwawa katika barabara ya Kilgoris kuelekea Nyangusu.