Madereva walalamikia ujambazi Baringo

  • | Citizen TV
    1,165 views

    Tume ya ugavi wa mapato (CRA) imesema kuwa mapato ya kaunti yamepungua kwa shilingi bilioni 157. CRA inasema kuwa kaunti zimeandikisha mapato ya shilingi bilioni 59 badala ya shilingi bilioni 216. mwenyekiti wa tume hiyo Mary Wanyonyi Chebukati kaunti hazijakusanya mapato kama inavyotarajiwa na hivyo sababu ya kutegemea pakubwa mgao wa pesa kutoka kwa serikali kuu. kaunti za Mombasa na Machakos zimetajwa kama bora zaidi kwa ukusanyaji wa mapato kutokana na mikakati iliyowekwa ya kuziba mianya ya ubadhirifu na ukusanyaji wa ushuru. aidha amesema pesa zinazotolewa za kusafirisha bidhaa kutoka kaunti moja hadi nyingine - CESS - zinahujumu ugatuzi.