Kiwanda kipya cha pamba chazinduliwa Mpeketoni, Lamu

  • | Citizen TV
    300 views

    Wakulima wa pamba katika Kaunti ya Lamu sasa wamepata afueni baada ya uzinduzi rasmi wa kiwanda kipya cha pamba katika Wadi Bahari, huko Mpeketoni, kaunti ya Lamu. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuboresha usindikaji wa pamba na kuimarisha kipato cha wakulima. Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Lee Kinyanjui, amesema kwamba kiwanda hicho kitaongeza usindikaji wa pamba, kubuni nafasi za ajira, na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi ya sekta ya nguo.