Maseneta watetea basari za taasisi za elimu

  • | Citizen TV
    326 views

    vuta nikuvute ya basari ikiendelea kuhusu magavana kutoa basari, maseneta sasa wanashinikiza kaunti ziendelee kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa shule za taasisi. Wito huo unajiri kutokana na hali ya switafahamu kufuatia kauli ya Mdhibiti wa Bajetikuwa serikali za kaunti hazina msingi wa kisheria wa kuwapa basari wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu, akisisitiza kuwa ni jukumu la serikali kuu. maseneta wanasema kuwa kaunti zinafaa kupewa mamlaka ya kusimamia fedha hizo kwa vile Magavana na wawakilishi wadi wako karibu zaidi na wakazi ikilinganishwa na wabunge ambao kazi zao ni za kutunga sheria.Maseneta hao walizuru bunge la Kaunti ya kilifi.