Vijana na wanaharakati wavamia bunge la Mombasa

  • | Citizen TV
    1,505 views

    Kizazaa kimeshuhudiwa nje na ndani ya majengo ya bunge la kaunti ya mombasa baada ya vijana wa kizazi cha GEN Z na wanaharakati wa kutetea haki kuvamia majengo hayo wakilalamikia mapendelezo ya bajeti mwaka 2025/2026. Vijana hao waliojawa na ghadhabu wanadai wakaazi wa mombasa hawajahusishwa katika mchakato huo na kutaka uwazi. Hali hii wanasema imechangia kwa changamoto zinazokumba kaunti ya mombasa. Vijana hao wanawalaumu wawakilishi wadi kwa kukosa kuwajibika na kuwahusisha katika mchakato wa bajeti. Karani wa Bunge la kaunti ya mombasa Salim Juma aliyepokea matakwa hayo na kuahidi kutoa mwelekeo jumanne wiki ijayo. Vijana hao wametishia kurudi tena iwapo matakwa hayi hayatasikizwa.