Wakazi wa Nakukulas, Turkana wapata hatimiliki za ardhi

  • | Citizen TV
    100 views

    Wakazi wa eneo la Nakukulas kwenye Kaunti ndogo ya Turkana Mashariki wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kusajili rasmi ardhi yao iliyokuw aimechimbwa mafuta na kampuni ya Tullow. Wakazi hao wamekabidhiwa hati miliki za ardhi na maafisa kutoka wizara ya ardhi. Sherehe ya kufana ya zoezi hilo ilifanyika huku wakazi wakisema watawapa fursa ya kukaa chini na kuelewana na mwekezaji yeyote anayetaka kuwekeza katika ardhi yao, ikizingatiwa kuwa eneo hilo lina utajiri wa mafuta.