Wakazi wa Namanga wanahofia mlipuko wa kipindupindu

  • | Citizen TV
    269 views

    Wakazi katika mji wa namanga, kaunti ya Kajiado wanaishi kwa hofu ya mlipuko wa kipindupindu, kufutia maji taka yanayotiririka hadi ndani ya mto Namanga. Wakazi hao wanadai maji hayo chafu yanatoka katika kituo cha forodha cha namanga, huku juhudi zao za kutaka idara ya afya ya umma kukomesha umwagaji wa maji hayo zikingonga mwamba. Wanasema wameiandikia wizara ya afya katika kaunti ya kajiado wakiitaka kuingilia kati ila kwa miezi minne sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.