Koti yasitisha uteuzi wa bodi iliyoteuliwa na rais Ruto

  • | Citizen TV
    260 views

    Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamefurahishwa na uamuzi wa Mahakama ya Juu uliotangaza kutupilia mbali kwa uteuzi wa Rais William Ruto wa wanachama wa kamati ya kitaifa ya Mabadiliko ya Tabianchi kuwa kinyume cha sheria na kinyume cha katiba. Kulingana na uamuzi huo, mahakama iligundua kuwa uteuzi huo ulipuuza michakato ya kisheria, ulikosa ushirikishi wa umma na kudhoofisha ushirikiano wa wadau mbalimbali katika Baraza la Kitaifa la Mabadiliko ya Tabianchi kama ilivyokusudiwa chini ya Sheria ya Mabadiliko ya Tabianchi, 2016.