Mzozo wa Shamba Olorieni, Kajiado

  • | Citizen TV
    223 views

    Viongozi kutoka kaunti ya Kajiado wanaitaka serikali iingilie kati na kutatua mzozo unaozingira shamba la Olorieni, lililoko Kajiado Mashariki ili kupunguza ongezeko la mgogoro baina ya wakazi na wanyapori ambao unazidi kuongezeka. Wanasema baadhi ya watu kupitia amri ya mahakama wamevamia shamba hilo na kujenga nyumba ambazo zimeziba njia ya wanyapori wanaotoka Mbuga ya Amboseli kuelekea eneo la Kyulu.