Tazama dereva wa pikipiki alivyonusurika kwenye ajali mbaya ya gari

  • | BBC Swahili
    4,088 views
    Onyo: video hii ina picha za kutatanisha Je unadhani uhasama kati ya wenye magari na bodaboda ni hapa kwetu tu? 😲💥 🎬🏍️ Mwendesha pikipiki alikuwa akavurumisha kitu kwa kasi akiwa anampelekea mteja chakula, ghafla gari likapinda kulia – boom! – akagonga gari lililokuwa likigeuza barabarani, akarushwa juu hewani kama mwigizaji kwenye “stunt ya filamu kama zile za Rambo”! Baada ya kugundua bado anapumua, jamaa akanyanyuka kama mchezaji wa WWE, akapiga mashini moto na kuendelea na safari kama hakuna kilichotokea! 😎👣 Ripoti zinasema hana majeraha makubwa. Na kilichomwokoa? Kofia ya usalama! Kwa hiyo ndugu zangu, si tu chakula kilifika salama – hata dereva wake alifika salama… kwa mtindo wa "Mission: Im-pikipiki!" 😂🍕🛵 Somo la leo? Kofia ya usalama si mapambo – ni kinga ya kichwa chako! 🪖 #bbcswahili #argentina #ajalibarabarani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw