Kifo hospitalini Mombasa

  • | Citizen TV
    2,088 views

    Familia moja katika kaunti ya Mombasa inalilia haki baada ya mpendwa wao kufariki kutokana na kile wanachodai kudungwa sindano isiyofaa. Familia ya Faith Anindo mama mjamzito inadai alienda hospitalini na tatizo la kipele lakini baada ya kudungwa sindano macho yaligeuka rangi ya njano na mwili kuanza kufura. Serikali ya kaunti ya mombasa imeanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo chake.