- 36,922 viewsDuration: 2:24Toka kutokea kwa vurugu za maandamano wakati wa uchaguzi mkuu nchini Tanzania, baadhi ya familia zimeelezea kupoteza wapendwa wao, ambapo baadhi wamethibitisha kuuawa huku wengine mpaka sasa bado hawajui wako wapi, baada ya kuwatafuta hospital hasa maeneo ya kuhifadhi maiti na vituo vya polisi. - BBC imezungumza na wahudumu wa afya wakiwemo madaktari kutoka hospitali binafsi na serikali, wanasema kuwa magari yamekua yakichukua miili na kupeleka maeneo yasiyojulikana. Aidha madakatari hao wameomba kutotajwa majina yao kutokana na hali ya usalama. BBC imemtafuta msemaji wa serikali ya Tanzania kujibu madai hayo bila mafanikio. - - # #bbcswahili #foryou #maandamano #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw