Wakazi kaunti ya Kirinyaga wanalalamikia kuhangaishwa na polisi katika maeneo ya burudani

  • | Citizen TV
    286 views

    Hali ya taharuki imetanda katika kaunti ya Kirinyaga kufuatia visa vya watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa usalama kuingia katika maeneo ya burudani usiku, kuwadhulumu wateja na kuharibu mali. Baadhi ya waathiriwa wanadai kuwa dhulma hizo zimekuwa zikitekelezwa kwenye operesheni za polisi na kuwalenga vijana. Na kama anavyoarifu Gatete Njoroge, viongozi wa kaunti ya kirinyaga wanamtaka waziri wa usalama kipchumba murkomen kuangazia suala hilo huku asasi za usalama zikisalia kimya.