Walimu wote nchini kupata nyongeza ya mishahara

  • | Citizen TV
    3,250 views

    Tunakunjua jamvi la nipashe wikendi kwa habari njema kwa walimu wote nchini ambapo sasa wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia kuafikiwa kwa nyongeza ya mishahara. Mkataba mpya wa maelewao ulioafikiwa kati ya vyama vya walimu na mwajiri wao -TSC umewaongezea mishahara kwa hadi asilimia 29.5. Sasa walimu wanaolipwa mshahara wa chini zaidi wa shilingi 23,000 utaongezwa hadi shilingi 29,000. Utekelezaji w amkataba huo utagharimu shilingi bilioni 33.8 na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne.