- 13,458 viewsDuration: 46sMamlaka katika jimbo la Kebbi kaskazini magharibi mwa Nigeria zinasema wanajeshi, polisi na watu wa kujitolea wanasaka maeneo ya misitu kuwafuata watu waliojihami waliowateka nyara wasichana zaidi ya ishirini kutoka shule ya bweni nchini humo Msemaji alisema kuwa gavana wa jimbo hilo alikuwa akipanga mikakati ya kuhakikisha wasichana hao wanaokolewa. Kebbi imeshuhudia ongezeko la utekaji nyara wa watu wengi unaofanywa na makundi yaliyojihami yanayotaka kikombozi. Jiunge na @midababirye mwendo wa saa tatu kamili katika Dira ya dunia kwa taarifa hii na nyengine nyingi. Tunapatikana mubashara kwenye ukurasa wa facebook na youtube, tafuta bbcswahili - - #bbcswahili #diratv #habari #nigeria #bringbackourgirls