Skip to main content
Skip to main content

BBC Africa Eye yagundua biashara haramu na ya siri ya viungo vya binadamu vinavyouzwa Sierra Leone

  • | BBC Swahili
    14,901 views
    Duration: 44:53
    Upekuzi wa BBC Africa Eye umegundua uwepo wa biashara haramu ya viungo vya mwili wa binadamu nchini Sierra Leone. Katika uchunguzi huo wa siri, mwandishi alijifanya mnunuzi anayetaka viungo hivyo kwa matumizi ya rituali za kishirikina ili kupata mafanikio ya kisiasa — na mtuhumiwa alionekana tayari kutekeleza ombi hilo. Waganga wa jadi nchini humo sasa wanajitahidi kurejesha heshima ya taaluma yao, wakishirikiana na polisi kukabiliana na matapeli wanaochochea biashara hii ya chini kwa chini. Hata hivyo, mauaji ya kimila hayarekodiwi kama kosa maalum, jambo linalofanya kiwango halisi cha matukio haya kubaki kitendawili. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw