Skip to main content
Skip to main content

Wabuni kola za chuma kukabiliana na chui

  • | BBC Swahili
    21,889 views
    Duration: 1:05
    Kijiji kilicho katika Pune, katika jimbo la Maharashtra magharibi mwa India, kimepata njia ya kipekee ya kupunguza mashambulizi ya chui. Baadhi ya watu katika kijiji sasa huvaa shanga zenye miba mikali wanapofanya kazi mashambani. Miba hiyo hulinda shingo na koo, ambavyo ni sehemu muhimu ambazo mnyama huyo hushambulia. Wakazi wengi wameanza kutumia shanga hizo kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi ya chui. Watu watatu wamefariki hivi karibuni, kulingana na Idara ya Misitu. - - #Bbcswahili #wanyamapori #wakulima #kinga