- 1,649 viewsDuration: 2:32Mahakama imeamrisha utekelezaji wa mkataba wa afya uliotiwa saini na marais William Ruto na Donald Trump wa Marekani usitishwe. Aidha Waziri wa Masuala ya kigeni, wa Afya na wa Fedha pamoja na mwanasheria mkuu wameagizwa kutotekeleza au kuzingatia kwa vyovyote vipengee vyote vya mkataba huo hadi kesi iliyowasilishwa iamuliwe. na kama anavyoarifu melita oletenges, Jaji Chacha Mwita amesema kwamba Ombi la Seneta wa Busia Okiyah Omtatah limeafiki mahitaji ya kisheria ya kusababishwa kusitishwa kwa mkataba huo kwa muda.