- 274 viewsDuration: 1:53Baadhi ya wazazi wameelezea kutoridhishwa kwao na matokeo ya shule za upili waliokoitwa wana wao wanaojiunga na gredi ya 10. Matokeo hayo yaliyotolewa kuanzia Ijumaa yamepokelewa kwa shauku kwani baadhi ya wanafunzi wameitwa katika shule za kutwa zilizoko nje na maeneo wanakoishi wazazi. Wizara ya elimu imesema kuwa kila mwanafunzi alipata matokeo kulingana na shule aliyochagua na kuwa fursa ya kuchagua shule mbadala itaanza Jumanne wiki ijayo.