Mahakama kuu imetoa agizo la kuzuia serikali kuanzisha hazina ya kitaifa ya miundombinu iliyopendekezwa, hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Agizo hilo lilitolewa na jaji Bahati Mwamuye jana jioni baada ya maombi yaliyowasilishwa na daktari wa upasuaji kutoka Nakuru, Dkt. Benjamin Gikenyi, Eliud Matindi na wengine, wanaopinga kuanzishwa kwa hazina hiyo kupitia agizo la rais la tarehe 15 mwezi Desemba mwaka 2025. Walalamishi hao wamesema hatua hiyo ya rais inahatarisha misingi ya katiba, ikiwemo ukuu wa Katiba, matumizi ya busara ya rasilimali za umma, uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa umma.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive