- 81,984 viewsDuration: 3:06Baadhi ya vijana waliohudhuria hafla ya kuwawezesha kiuchumi katika ikulu ya rais, wiki jana, wamejitokeza kudai hawakupokea pikipiki walizoahidiwa pamoja na vifaa vingine. Sasa wanadai kuhofia maisha yao baada ya kupokea vitisho walipochapisha video mtandaoni kulalamikia swala hili. Vijana hao wamekosoa mpango huo na kusema iwapo kuna yeyote aliyepokea pikipiki hizo pamoja na stakabadhi za umiliki, ajitokeze.