Familia mbili huko Mombasa na Isiolo zinasononeka kutokana na kutekwa nyara kwa wapendwa wao. Katika tukio la hivi punde, mwanamke mmoja katika eneo la Sisi kwa Sisi huko Soweto, Kaunti Ndogo ya Changamwe huko Mombasa, anasema wanaume wenye silaha walimteka nyara mumewe wa miaka 44 siku ya Krismasi na kuondoka naye kwa gari la kubebea mizigo lisilo na nambari za usajili. Na huko Isiolo, polisi wa akiba wa kitaifa alichukuliwa na wanaume waliokuwa wamevaa barakoa zaidi ya wiki moja iliyopita na hadi sasa hajapatikana.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive