- 8,641 viewsDuration: 4:03Halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani(NTSA) imetekeleza msako kwenye barabara kuu ya Nairobi Eldoret katika juhudi za kupunguza ajali barabarani. Msako huo unaotekelezwa kwa ushirikiano na maafisa wa trafiki katika kaunti ya Uasin Gishu, unalenga uendeshaji mbaya wa magari, uchovu wa dereva na umiliki wa leseni zisizo halali. Magari 25 tayari yamenaswa kutokana na kuendeshwa kwa kasi, yakiwemo magari 18 ya kibinafsi ambayo madereva wake wanatarajiwa kufikishwa mahakamani. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive