Skip to main content
Skip to main content

Wazazi wapinga ujenzi wa sanamu ya Mbunge shuleni

  • | Citizen TV
    10,771 views
    Duration: 3:27
    Wazazi na wakazi wa Acherspost samburu mashariki,wameshtumu vikali kujengwa kwa sanamu ya mbunge wa eneo bunge hilo Jackson Lekumontare katika shule ya upili ya wasichana ya UASO. Wazazi hao wanadai shilingi milioni kumi na tano za umma zilifujwa katika kufadhili ujenzi wa sanamu hiyo,. Hata hivyo, usimamizi wa shule hiyo unadai ulitumia shilingi laki moja unusu kujenga sanamu hiyo kama shukurani kwa juhudi za mbunge huyo za kuboresha viwango vya elimu. Wazazi wa shule hiyo sasa wanaitaka tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kuchunguza kisa hicho.