Skip to main content
Skip to main content

Umiliki wa ardhi wazua mgogoro Eastleigh

  • | KBC Video
    1,415 views
    Duration: 3:03
    Mzozo wa ardhi unaotokota kwenye mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi umesababisha serikali kuingilia kati baada ya baadhi ya wakazi kuibua wasiwasi kuhusiana na madai ya unyakuzi wa ardhi hiyo ambayo ilikuwa imedhamiriwa kunufaisha umma, ukiwemo ujenzi wa vituo vya kuwahudumia watu walio na ulemavu pamoja na watoto klutoka familia zisizojiweza. Kipande hicho cha ardhi kinachokumbwa na utata kilicho karibu na shule ya upili ya wavulana ya Starehe kimekuwa kitovu cha ubishi kati ya usimamizi wa kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalum na mstawishaji wa kibinafsi kutoka sehemu hiyo ambaye alikodisha ardhi hiyo mwaka-2020 japo kwa sasa anadai kuimiliki. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive