- 1,355 viewsDuration: 1:22Rais William Ruto amewaonya vikali walimu wakuu kuhusu kuwalazimisha wazazi kununua sare za shule kwenye maduka maalum au shuleni. Rais Ruto amesema kuwa suala la sare za shule limeanza kuendeleza ufisadi katika sekta ya elimu huku baadhi ya shule zikiwalazimisha walimu kulipa hadi shilingi elfu arobaini kugharamia sare. Rais amesisitiza kuwa wanafunzi wanaojiunga na gredi ya kumi waruhusiwe shuleni hata iwapo hawana sare za shule za sekondari ya juu.