Waziri wa afya Aden Duale amesisitiza kuwa mamlaka ya afya ya jamii SHA, haitalipa madeni ghushi kwa huduma ambazo hazikutolewa kwa wagonjwa na hospitali zinazodai mamlaka hiyo.
Duale amesema madeni hayo lazima yafanyiwe ukaguzi wa kina ili kubaini uhalisi wake kabla ya malipo hayo kufanyika. Akizungumza mjini Garissa, Duale amesema mamlaka hiyo imelipa karibu bilioni 75 ikiwemo mpango wa afya ya wafanyikazi wa umma, huduma za dharura na hazina ya magonjwa sugu akitoa onyo kwa hospitali zinazolipisha huduma ya afya ya misingi kuwa zitachukuliwa hatua ya kisheria.