Serikali inawekeza katika ustawishaji wa miundombinu ya elimu, mafunzo ya walimu na mifumo ya miongozo ya kitaaluma ili kufanikisha mpito wa mfumo wa elimu ya umilisi-CBE, ukiwemo usajili unaotarajiwa wa zaidi ya wanafunzi milioni-1 kwenye taasisi za elimu ya juu kufikia mwaka-2029. Akizungumza wakati wa kongamano la kwanza la kitaifa la kitaaluma katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta-KICC jijini Nairobi, katibu katika idara ya elimu ya juu Beatrice Inyangala, alisema mageuzi katika ukuzaji wa mtaala tayari yanaendelea kutekelezwa katika azma ya kufanikisha utekelezaji wa mfumo huo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive