- 12,949 viewsDuration: 46sTazama Meya kutoka nchini Ufilipino alivyonusurika jaribio la nne la kuuawa hivi karibuni, baada ya shambulio la kombora kulenga gari lake mchana kweupe. Mamlaka za eneo za eneo la Shariff Aguak zilisema kupitia chapisho la Facebook kwamba Meya Akmad Mitra Ampatuan alinusurika, lakini kwa mujibu wa shirika la habari GMA Ufilipino, walinzi wake wawili walijeruhiwa. Hili ni jaribio la nne la kuvizia meya huyo katika miaka ya hivi karibuni. #bbcswahili #filipino #Ufilipino Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw