Skip to main content
Skip to main content

Wafugaji Kimalel watishia maandamano kufuatia malipo ya mifugo kuchelewa zaidi ya miezi miwili

  • | Citizen TV
    316 views
    Duration: 2:33
    Wafugaji wa mbuzi waliouza mifugo yao katika soko la mbuzi la Kimalel mwezi disemba wamelalamikia kutopewa malipo yao, takriban miezi miwili baada ya mifugo yao kuuzwa. Wanatishia kuandamana hadi katika ofisi za gavana wa kaunti hiyo kushinikiza malipo yao au warejeshewe mbuzi wao. Wafugaji hao wanadai matapeli waliingilia soko hilo na kujilipa kabla ya wafugaji halali kulipwa.