- 15,567 viewsDuration: 3:59Kinara wa Chama cha ODM Oburu Oginga amesema kuwa chama hicho hakina nia ya kuchukua kiti cha naibu rais katika mazungumzo yanayoendelea ya kutafuta ushirikiano wa kisiasa na UDA kwenye uchaguzi mkuu ujao. Akizungumza kwenye utoaji wa fedha kwa vijana chini ya mpango wa NYOTA huko Kisumu, Oburu alisema lengo la ODM ni kupata nafasi zenye mshiko kwenye serikali ijayo. Aidha Rais William Ruto, ambaye aliongoza hafla hiyo, amesema ushirikiano wao utaleta usawa nchini.