- 215 viewsDuration: 2:20Wakenya zaidi ya 530,000 wamepata ajira nje ya nchi katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita kupitia mpango wa serikali wa Kazi Majuu. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu wa idara ya Masuala ya Ughaibuni Roseline Njogu. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya lugha ya Kijerumani katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Meru, Njogu aliwaonya Wakenya wanaotafuta kazi ng'ambo kuwa waangalifu dhidi ya maajenti bandia.