- 2,906 viewsDuration: 2:51Makabiliano yalizuka kati ya polisi na wafanyabiashara mtaani Ruai, jijini Nairobi, baada ya juhudi za kuwaondoa katika eneo lililotengewa ujenzi wa barabara kutibuka. Wafanyabiashara walifunga barabara ya Eastern bypass wakipinga kuhamishwa hadi pale soko jipya litakapojengwa. Aidha wanadai ardhi iliyotengwa kwa ujenzi wa soko imetekwa na wahuni na kwamba hakuna soko lililojengwa.