- 1,476 viewsDuration: 2:01Spika wa bunge la seneti Amason Kingi sasa anataka mazungumzo kufanywa kati ya magavana na maseneta kufuatia tofauti za punde zilizoibuka. Akizungumza eneo la Soy kaunti ya Uasin Goshu, Kingi amesema malumbano hadharani hayatasuluhisha tofauti zilizoko. Msimamo wa Spika Kingi unajiri huku Gavana wa Narok Patrick Ole Ntutu amefika mbele ya kamati ya uhasibu ya bunge la seneti kuhojiwa kuhusu matumizi ya kaunti yake. Ntutu amefika mbele ya kamati hiyo, siku moja baada ya magavana kutishia kutofika mbele yao kwa kuwahangaisha. Kwenye kikao hicho, Mwenyekiti Moses Kajwang amesema magavana ni lazima watii amri wanapotakiwa kufika seneti