- 6,202 viewsDuration: 3:02Kizaazaa na fujo zilishuhudiwa siku kutwa katika eneo la mathira kaunti ya Nyeri, ambapo polisi na wakazi wa Kijiji cha Rititi walikabiliana vikali. Hii ni baada ya wakazi kuopoa mwili wa mtoto wa miaka 9, uliokuwa umetupwa chooni. Mtoto huyo, Shantel Waruguru aliyekuwa ameripotiwa kutoweka jumamosi, alipatikana amekatakatwa na kutupwa chooni humo. Wakazi pia wlaiteketeza nyumba ya mshukiwa na nyanya ya mtoto huyo wakidai kuwa waili hao walishirikiana kujaribu kuficha mwili.